Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Yakubu Mohamedi, amekabidhi rasmi Bendera ya Taifa kwa Maafisa na Askari wanamichezo wapatao 90 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaotarajia kushiriki katika michezo ya Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 13 hadi 23 Aug 19 nchini Kenya.
Michezo hiyo itashirikisha nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ikiwamo Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini pamoja na wenyeji Kenya.
Luteni Jenerali Yakubu Mohamedi kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi amemkabidhi rasmi Bendera Mkuu wa Msafara Meja Jenerali Sharif Othman ambaye pia ni Mkuu wa Kamandi Vikosi Chini ya Makao Makuu ya Jeshi kuashiria utayari wa kuanza safari ya kuelekea nchini Kenya kwenye mashindano hayo
Timu za wanamichezo wa JWTZ zitakazopeperusha bendera ya Taifa nchini Kenya ni pamoja na mpira wa Miguu, mpira wa Wavu, mpira wa Pete, mpira wa Kikapu na Riadha.
Akizungumza na wanamichezo na Viongozi wa Timu hizo Luteni Jenerali Yakub Mohamedi amewataka wawakilishi hao kwenda kushindana na kurudi na mataji mbalimbali huku akisisitiza kuendeleza Nidhamu na ushirikiano ndani na nje ya uwanjaTanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.