Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Salum Haji Othman amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM), ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Baraza hilo,Navy Captain Robert RecchieUpanga,Jijini Dar es Salaam .
Katika mazungumzo hayo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, ameukaribisha Ujumbe huo hapa nchini na kuwaeleza kutumia fursa waliyoipata kutembelea vivutio mbalimbali vya utaliivilivyoko hapa nchini.
Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM), Navy Captain Robert Recchie, amelishukuru JWTZ kwa mapokezi na maandalizi ya hali ya juu kuelekea kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza hilo Duniani.
Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 14 Mei 2024 Jijini Dar es Salaam ukiwashirikisha zaidi ya Wajumbe 300 kutoka Majeshi mbalimbali Duniani.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.