Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali James Mwakibolwa amewataka Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma wa Jeshi hilo kufanya kazi kwa juhudi, maarifa, nidhamu na weledi wakati wanapotekeleza majukumu yao.
Aidha Luteni Jenerali Mwakibolwa amesisitiza kuwa Wanajeshi wanatakiwa kubadilika kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuwa na Jeshi imara. Aliyasema hayo wakati akizungumza na Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma wa Makao Makuu ya JWTZ, Dar es Salaam kwa niaba ya Wanajeshi wote nchini.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.