Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Kanali Ramadhani Dogoli azungumzia uzinduzi wa Ukuta uliojengwa kuzunguka machimbo ya madini aina yaTanzanite yaliyopo Mererani Mkoani Manyara.
Akizungumza na waandishi wa habari Kanali Dogoli amesema uzinduzi huo utafanyika rasmi kesho April 06, 2018 Mererani. Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha amewataka waandishi wa habari kuandika habari kwa usahihi na umuhimu wa wanahabari kujua majina na vyeo vya kijeshi . Pia amewakumbusha wananchi kupitia waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kuandikishwa JWTZ na namna ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT).
Kanali Dogoli amewataka wananchi kutokubali kutapeliwa na watu wanaoahidi kutoa nafasi Jeshini.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.