Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Yakubu Mohamed amempokea Mwambata Jeshi toka Malawi Kanali Orton Msukwa, katika yaliyokuwa Makao Makuu ya Jeshi, Upanga jijini Dar es Salaam tarehe 7 Disemba 2020.
Kanali Msukwa alifika kujitambulisha kwa uongozi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kuanza kazi.
Ujio wa kiongozi huyo wa kijeshi ni mwendelezo wa uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Mataifa haya mawili.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.