Timu ya Mpira wa Pete ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo tarehe 17 August 2019 imeendeleza wimbi la ushindi katika Mashindano ya Majeshi yanayoendelea Nchini Kenya baada ya leo kuifunga timu ya Jeshi la Burundi kwa jumla ya magoli 99-16.
Katika mchezo uliopigwa katika Uwanja waShule ya Fedha hapa mjini Nairobi, Tanzania ilionesha kuwamudu vema wapinzani wao toka kipindi cha robo ya kwanzabaada ya kuwafunga magoli 38-4.
Aidha, katika robo ya pili Tanzania ikiongozwa na mfungaji wake mahili Koplo Mwanaidi Hassan iliongeza wimbi la magoli nampaka wanakwenda mapumziko Tanzania ilikuwa ikiongoza kwa jumla ya magoli 49-7.
Huu ni mchezo wake wa pili kwa Timu hiyo, na imefanya vizuri katika michezo yake yote. Katika mchezo wa kwanza iliweza kuifunga Timu Jeshi la Rwanda kwa jumla ya magoli 66-16.
Mwaka huu katika mashindano haya jumla ya nchi Wanachama sita zimeshiriki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini na kuna jumla ya michezo mitano itashindaniwa ikiwa ni Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu na Riadha.
Mara ya mwisho mashindano haya yalifanyika nchini Burundi na Tanzania ilinyakua nafasi ya kwanza katika mchezo huu wa Mpira wa Pete.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.