• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Ngome yazidi kung'ara BAMMATA

Ngome yazidi kung'ara BAMMATA Posted On: Friday, 12th September 2025

Timu za Ngome zinazomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania zimezidi kung'ara katika mashindano ya Michezo mbalimbali ya Majeshi (BAMMATA) ambayo yanafanyika mjini Zanzibar.

Baadhi ya michezo ambayo inaongoza hadi sasa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa mikono (handball), mpira wa pete pamoja na riadha.

Katika michezo iliyofanyika jana tarehe 11 Agosti 25, kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu timu ya Ngome ilifanikiwa kuifunga timu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) goli 1-0 mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung.

Mchezo mwingine ulikuwa ni mpira wa kikapu uliozikutanisha timu za Ngome na JKT ambapo Ngome iliibuka kidedea kwa kuichapa JKT alama 81 dhidi ya 57.

Kwa upande wa mchezo wa wavu uliozikutanisha timu za Ngome na Polisi katika uwanja wa Amani, Ngome ilishinda jumla ya seti 3-0 na kuzidi kujiweka nafasi ya kufanya vizuri.

Kwa upande wa mchezo wa riadha, timu ya Ngome imeendelea kuongoza Mita 100 fainali ya wanawake na kufuzu medali ya dhahabu huku timu ya riadha Ngome Wanawake Mita 5000 ikishika nafasi ya kwanza, na pia timu ya riadha Ngome wanaume na Wanawake Mita 10,000 .

Matokeo haya yanaipa timu ya Ngome kuwa na uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa wa mshindi wa jumla.

Habari Mpya

  • Ngome yazidi kung'ara BAMMATA

    Ngome yazidi kung'ara BAMMATA

    tokea masaa 13
  • Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi  Shule ya Polisi Jeshi Mafinga

    Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Shule ya Polisi Jeshi Mafinga

    tokea masaa 13
  • Mashindano ya BAMMATA yazinduliwa

    Mashindano ya BAMMATA yazinduliwa

    tokea siku 5
  • Mkuu wa Majeshi ya UAE afanya Ziara Tanzania

    Mkuu wa Majeshi ya UAE afanya Ziara Tanzania

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 3
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.