Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo Novemba 11 amefanya ziara fupi katika kikosi cha Usafishaji cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo jijini Dar es salaam na kujionea utayari wa kikosi hicho katika kutekeleza majukumu yake kijeshi na kitaifa pindi itakavyohitajika.
Rais Magufuli akiwa kikosini hapo alipata fursa ya kutembelea magari yenye uwezo wa kubeba uzito tofauti yanayotumika katika kutekeleza majukumu yake.
Aidha aliliagiza Jeshi liwe tayari katika zoezi aliloliita "Operesheni Korosho" linalotarajiwa kufanyika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga na Pwani.
Alisema " zoezi hilo litafanyika endapo agizo la Serikali la kuwataka wanunuzi wa Korosho kununua zao hilo kwa muda uliopendekezwa kushindikana.
Rais Magufuli alilipongeza Jeshi kwa kuwa mfano mzuri kwa Majeshi mengine Barani Afrika kwa utendaji kazi wake na kuwa na historia nzuri ya kupigania uhuru wa Bara la Afrika na kuwa historia hiyo haitafutika kamwe.
Vile vile alisisitiza umuhimu wa Serikali kuzidi kuliongezea nguvu JWTZ katika nyanja ya usafirishaji.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.