Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuliamefanya uzinduzi wa Vizimba 9 na Mabwawa 18 ya Samaki aina ya Sato yanayomilikiwa na Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Mjini Musoma tarehe 6 Septemba 18
Akizungumza baada ya uzinduzi huo Dkt. Magufuli amelipongeza Jeshi hilo kwa kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali na kuahidi kukisaidia Kikosi hicho ili kuendeleza mradi huo.
Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema Jeshi lipo kwenye mpango wa kujenga kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki kwani hii ni hatua ya mwanzoni ikiwa ni katika kulifanya Jeshi lisiwe tegemezi kutoka Serikalini.
Akizungumza baada ya kukaribishwa na mwenyeji wake Waziri mwenye dhamana ya Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina,amelihakikishia Jeshi kuwa ofisi yake ipo wazi wakati wote kutoa msaada wa kitaalamu pindi unapohitajka.
Aidha,Mkuu wa Kikosi Luteni Kanali Mshashi alimueleza Rais kuwa mradi huo mpaka sasa umetumia zaidi ya shilingi milioni mia mbili na kuwa mradi huo utakapoanza kutoa samaki unatarajia kuzalisha shilingi milioni 700 kwa mwezi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.