Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt John Pombe Magufuli ametunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Julai 7, 2018 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Jumla ya Maafisa 121 walipata mafunzo na kahitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) kilichopo jijini Arusha. Kati yao kuna waliotoka nchi rafiki kama vile Uganda, Rwanda na eSwatini na wengine wawili walipata mafunzo yao nchini India.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli tangu aingie madarakani mwaka 2015 ametunuku Kamisheni kwa mara ya sita huku ikiwa ni mara yake ya nne kutoa Kamisheni katika Viwanja vya Ikulu.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.