Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua jengo jipya la Chuo Cha Ulinzi cha Taifa(NDC) kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam. Tarehe 14 Novemba 21 Mhe. Rais alizindua jengo hilo ambalo limejengwa kwa ufadhili wa serikali ya China kwa gharama ya shilingi bilioni 57.
Akizindua jengo hilo Mhe. Rais Samia alisema ujenzi wa chuo hicho umelisaidia jeshi na taifa kwa kuokoa fedha nyingi zilizotumika kusomesha wanafunzi nje ya nchi kwa gharama kubwa, hivyo serikali itaelekeza fedha hizo kwenye shughuli za maendeleo.
“Pamoja na kupata majengo tunatakiwa kuboresha elimu katika sekta ya ulinzi na usalama nchini, sambamba na mitaala na mbinu za utoaji mafunzo kuendana na wakati kukidhi mahitaji ya fani husika” alisema Mhe Rais.
Aidha, Rais Samia ameishukuru serikali ya Watu wa china kwa msaada wa majengo hayo ambayo yatasaidia kuongeza idadi ya wadahiliwa, na kutoa fursa kwa chuo kuendesha kozi Zaidi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.