Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 118 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika kwenye Chuo cha Kijeshi cha Maafisa Monduli, Arusha tarehe 22 Novemba 2021.
Kati ya Maafisa hao wapya, 99 ni maafisa wanaume na 19 ni wanawake.
Mkuu wa Chuo cha Kijeshi Monduli Brigedia Jenerali Jackson Jairos Mwaseba alisema Maafisa wapya waliotunukiwa Kamisheni wamefanya mafunzo yao hapa nchini na nje ya nchi wakiwemo marubani na injinia wa ndege.
Mbali na kutunuku Kamisheni, Rais na Amiri Jeshi Mkuu amewatunuku shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi maafisa wapya 61.
Akiongea na maafisa wapya hao Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Salvatory Venance Mabeyo amewataka Maafisa wapya kukiishi kiapo walichokiapa mbele ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu maisha yao yote.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.