Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo Aprili 06, 2018 amezindua ukuta uliojengwa kuzunguka migodi ya Tanzanite Mererani mkoani Manyara.
Katika hotuba yake Rais Magufuli amelisifu Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kukamilisha ujenzi wa ukuta huo ndani ya muda na kwa weledi mkubwa.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo akiwemo Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi yaUlinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo, Mawaziri pamoja na wabunge na makamanda wa JWTZ.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.