Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuwa na jeshi lililo imara kulinda mipaka ya nchi ya Tanzania.
Ametoa pongezi hizo alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Kabla ya hotuba hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan alikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake lililokuwa linaongozwa na vikundi kutoka JWTZ pamoja na vyombo vya usalama.
Maadhimisho hayo yalipambwa na maonesho kutoka vikundi mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na makomando wa JWTZ
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.