Sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimefanyika tarehe 26 Aprili 2018 katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,Dkt. John Pombe Magufuli.
Tarehe kama ya leo Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Waasisi wa Mataifa haya mawili, Hayati baba wa Taifa, Mwlimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Shekh Abeid Karume kutiliana saini mwaka 1964. Muungano wetu umetimiza miaka 54 ukiwa na kauli mbiu inayosema ''Muungano wetu ni mfano wa kuigwa duniani, tuuenzi, tuulinde, tuudumishe kwa maendeleo ya Taifa letu''
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.