Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo Julai 25,2018 limeadhimisha kumbukizi ya siku ya mashujaa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii nchini kote.
Katika kuadhimisha siku hii Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo amewatembelea wagonjwa wanaopata matibabu kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, kushiriki kufanya usafi eneo la Lugalo na baadae alipata fursa ya kuongea na Wananchi waliojitokeza kupima afya zao katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni moja ya huduma ya kijamii iliotolewa na Jeshi katika kuadhimisha siku ya Mashujaa mwaka huu.
Mkuu wa Majeshi amewaomba wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani huduma hiyo itatolewa mpaka Julai 28,2018.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.