Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania pamoja na Wizara ya Ulinzi ya Ethiopia zimesaini mkataba wa ushirikiano wa ulinzi leo hii jijini Dar es Salaam kwenye kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Upanga.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Alfred Kapinga kwa upande wa Tanzania na Kanali Yenus Mulu Takele kwa upande wa Ethiopia.
Ushirikiano huo wa nyanja mbalimbali za ulinzi umejikita zaidi kwenye mafunzo, ulinzi wa amani, ubadilishanaji wa sekta ya sayansi na teknolojia na vita dhidi ya ugaidi pamoja na uchangiaji wa majeshi kwenye Jeshi la Afrika.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.