Tanzania na Jamhuri ya Comoro zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano kwenye nyanja za kijeshi.
Utiaji huo wa saini umefanywa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Stergomena Tax na Waziri wa Ulinzi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Visiwa vya Comoro Mhe Yousoufa Mohamed Ali jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kutiliana saini mkataba huo, Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe Stergomena Tax amesema mkataba huo utaongeza na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili hasa katika nyanja ya kiulinzi, kiusalama, kimafunzo, uzalishaji mali pamoja na tiba.
Naye Waziri wa Ulinzi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Visiwa vya Comoro Yousoufa Mohamed Ali ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa na ushirikiano mzuri na nchi yake na kuahidi kuendelea nao kwani una manufaa kwa pande zote mbili.
Tanzania na Comoro ni marafiki wa muda mrefu na zimekuwa zikishirikiana katika nyanja mbalimbali.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.