Takribani ni mwezi mmoja umepita sasa toka Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imeitoa Harambee Stars kwenye Michuano ya kuwania kufuzu kwenye Mashindano ya CHAN. kwa mikwaju ya Penati.
Tarehe 13 Agosti mwaka huu Michezo ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki yalizinduliwa rasmi na Waziri wa Ulinzi wa Kenya Balozi Raychelle Omamo kwa kuwataka washiriki kutambua kuwa michezo hiyo inalengo la kuwafanya Wanaafrika Mashariki kuendeleza hali ya Amani na utulivu iliyopo baina nchi wanachama kwa kupitia michezo.
Katika mwendelezo wa michezo hiyo leo tarehe 19 Agosti 2019, Tanzania ikiwakilishwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linashiriki kwa kupeleka timu tano za michezo tofauti. limeweza kushiriki katika michezo mitatu.
Katika mchezo wa Mpira wa miguu Tanzania imeweza kuwafunga wenyeji Ulinzi Stars2-1. Mchezo ulionza katika majira ya saa kumi na nusu Tanzania walikuwa wa kwanza kuliona lango la Ulinzi Stars, katika dakika (08) lililofungwa na kiungo wake machachali Kelvin Nashoni baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Samweli Kamuntu na kuachia shuti kali lilikwenda nyavunimoja kwa moja.
Kipindi cha pili Kenya walifanya mabadiliko kwa kumwingiza Enosi Ochieng, mabadiliko hayo m yaliweza kuwasaidiana kupata goli katika dakika (53). Tanzania nao walifanya mabadilikokatika dakika (58) kwa kuwatoa Prosper Nkwama na kumwingiza Najim Magulu, Mgandila Shabani/Hassan Gumbo na Samwel Kamuntu alimpisha Hussein Nyamanduru (Agogo). Mabadilko hayo yaliendelea kuwaweka pabaya wenyeji kwani mnamo dakika ya (74) ya mchezo Nahodha wa wa Timu ya Tanzania Fuluzulu Maganga aliweza kuipatia timu yake bao la pili na la ushindi na kuwaacha wenyeji wakiduwaa wasijue la kufanya.
Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa Waziri wa Ulinzi wa Kenya Balozi Raychelle Omamo aliyeambatana na Makamu Mkuu wa Majeshi ya Kenya Luteni Jenerali Robert Kibochi, Meja Jenerali (wa kwanza nchini Kenya) Fatuma Mohammed, Mkurugenzi wa Michezo JWTZ Kanali Erasmus Bwegoge na viongozi wengine.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.