Timu ya Mpira wa Miguu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imefanikiwa kuilaza Timu ya Jeshi la Burundi Muzinga FCkwa ushindi mabao 7-0 mchezo wake wa kwanza katika Mashindano ya Majeshi ya Nchi za Afrika Mashariki yanayoendelea nchini Kenya.
Katika mchezo ulionza majira ya saa tisa jioni Tanzania ilikuwa ya kwanza kufumania nyavu za Burundikatika dakika ya nane ya mchezo kupitia kwa Mshambuliaji wake Samweli Kamuntu.
Baada ya bao hilo Tanzania iliendelea kulishambulia lango la Muzinga FC na kufanikiwa kuongeza goli la pilikatika dakika (34) kupitia kwa Mshambulia wake Fuluzulu Maganga ambaye alionekana kuwa mwiba kwa Burundi.
Mnamo dakika ya (45) Tanzania iliongeza goli la tatu kupitia kwa winga wake Anwary Kilemile aliyewatoka mabeki wa Burundi na kuachia mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango wa Burundi na kutinga wavuni.
Kipindi cha pili Burundi waliweza kupata goli la kwanza katika ( 47 ) na dakika tatu baadae(50) waliongeza goli la pili.
Hali hiyo iliwaamshawachezaji wa Timu ya Tanzania na kuanza kulishambulia lango la Timu ya Muzinga FC. Mashambulizihayo yaliweza kuzaa matunda kwakuongeza goli la nne kupitia kwa Edward Songo lililopatikana katika dakika (54).
Fuluzulu Maganga tena aliweza kuipatia Tanzania bao la Tano katika dakika (63) na kukamilisha mabao matatu aliyoyafunga kwenye mchezo huo na kuondoka na mpira. Dakika saba baadae Burundi walijipatia goli la tatu.
Dakika (86) Edward Songo tena aliinua Tanzania kwa kufunga goli la Saba, na hivyo kufanya Tanzania kutoka uwanjani kifua mbele kwa magoli 7-3.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.