Kikosi cha 7 cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania (TANZBATT-07) kinachohudumu katika Ulinzi wa Amani Jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC kimehitimisha rasmi majukumu yake na kukabidhi jukumu hilo kwa Kikosi cha nane 8 (TANZBATT-08) ambacho kimewasili tarehe 09 January 2021, tayari kwa kupeperusha Bendera ya Taifa katika ardhi ya DRC kwenye Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha kujibu Mashambulizi (Force Intervention Brigade) MONUSCO.
Kamanda Kikosi cha 7 Luteni Kanali John Ndunguru (kulia) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Kamanda Kikosi cha 8 Luteni Kanali Fortunatus Nassoro.
Baada ya kukabidhi Bendera hiyo kwa Gwaride Maalum, Kamanda Kikosi cha 7 Luteni Kanali John Ndunguru amesema kufikia hatua hiyo ni kutokana na umoja na mshikamano uliopo baina Maafisa na Askari walinda Amani.
Aidha, Kamanda Kikosi cha 8 Luteni Kanali Fortunatus Nassoro amesema atayaendeleza yote yaliyofanywa na Kikosi kinachoondoka, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Walinda Amani na Raia
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.