Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo anasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Dagobert Komba (Mstaafu)kilichotokea tarehe 29 April 2018 katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo jijini Dar es salaam.
Marehemu Brigedia Jenerali Komba (mstaafu) alizaliwa mwaka 1949 mkoani Ruvuma. Alijiunga na JWTZ mwaka 1971 na kutunukiwa kamisheni mwaka 1973. Wakati wa utumishi wake Marehemu Brigedia Jenerali Komba (mstaafu) alishika madaraka mbalimbali. Hadi anastaafu alikuwa Mkuu wa Tawi la Mipango na Maendeleo Jeshini(SPD).
Marehemu Brigedia Jenerali Komba(mstaafu) aliagwa tarehe 2 Mei, 2018 katika hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo na kusafirishwa kwenda Mbinga mkoani Ruvuma kwa mazishi yatakayofanyika leo tarehe 04 Mei 2018
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.