Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha miaka mitano ijayo leo Novemba 5, 2020 wakati wa sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Akizungumza na wananchi wa Tanzania akiwa katika uwanja wa Jamhuri, Dkt. Magufuli amesisitiza kuilinda Amani tulionayo na kuendelea kufanya kazi ili kuleta maendeleo “Uchaguzi sasa umekwisha, jukumu kubwa na muhimu lililo mbele yetu ni kuendeleza jitihada za kulijenga na kuleta maendeleo kwa nchi yetu” amesema Dkt. Magufuli.
Nae Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museven akizungumza wakati wa sherehe hizo amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika Mashariki kuimarisha usalama na kushirikiana kibiashara.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.