Serikali ya Ujerumani kupitia Balozi wake hapa nchini, Dkt.Waechter imekabidhi Hospitali ya Kanda ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
Akikabidhi funguo ikiwa kama ishara ya makabidhiano kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Balozi Waechter alimesema kuwa Hospitali hiyo ni moja ya mikataba kati ya Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani na Wizara ya Ulinzi ya Tanzania kupitia Sekta ya Afya.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi aliiomba Serikali ya Ujerumani kuendelea kutoa msaada kwa Jeshi kwa kuwa Hospitali hizo hazihudumii Wanajeshi pekee bali zinasaidia na wananchi.
“Serikali ya Ujerumani imekuwa ikitusaidia sana,kwani imetusaidia katika ujenzi wa Chuo cha Tiba, Hospitali za Mwanza, Mbeya na Tabora na vifaa vya tiba,pia niwashukuru kwa kuongeza muda wa mradi” Alisema Waziri Mwinyi.
Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo alisema kuwa mpaka kukamilika kwa Hospitali hiyo kumegharimu shilingi bilioni 5.6. kiasi hicho cha fedha kimetolewa na Serikali ya Ujerumani kutokana na Uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili.
Aidha, Mkuu wa Tawi la Tiba Jeshini, Meja Jenerali Denis Janga alisema huduma za matibabu zitaanzamapema ambapo kutakuwa na wataalam wa idara zote ikiwemo meno, Mama na Mtoto na picha (X-Ray) huku ikiwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 300 pamoja na kulaza wagonjwa 50 kwa siku
Uwepo wa Hospitali hiyo Mkoani humo, kutasaidia kuimarisha afya za Wananchi, na kutapunguza gharama na idadi ya wagonjwa kwa kuwapeleka nje ya Mkoa kwa ajili ya matibabu
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.