Tarehe 29 Mei ni siku ya Walinda Amani ambayo huadhimishwa kila mwaka Duniani kote. Kauli mbiu ya Maadhimisho kwa mwaka huu ni “Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya Huduma na Kujitoa”.
Tanzania kama mwanachama wa Umoja huo imeadhimisha kumbukumbu hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga ambapo alitoa historia ya Tanzania katika ushiriki wake kwenye shughuli hizo na kusema kuwa Tanzania ilianza rasmi kushiriki katika ulinzi wa amani mwaka 2006.
“Hii ni siku maalum kwa Tanzania na Majeshi ya Umoja wa Mataifa ambapo Tanzania ilianza kushiriki Ulinzi wa Amani kuanzia mwaka 2006, ni takribani miaka 12 ya ushiriki wake. Katika muda huo watu walitambua umuhimu wa Tanzania kushiriki kwake katika Ulinzi wa Amani kwa kupeleka Majeshi yetu kwa mara ya kwanza nchini Lebanon” alisema Balozi Mahiga.
Tanzania imekua ikisifika katika shughuli za Ulinzi wa Amani kupitia majeshi yake katika nchi mbalimbali. Mpaka sasa majeshi yetu yapo nchini Sudan katika jimbo la Darfur, Lebanon, Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.