Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), leo tarehe 16 Aprili 2019 limefanya Uzinduzi wa ujenzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam kwa kuweka jiwe la msingi. Mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dkt. Hussein Mwinyi.
Dkt. Mwinyi amesema kuwa ujenzi wa chuo hicho umekuja baada ya hitajio kubwa la kozi mbalimbali zinazoendeshwa chuoni hapo. Aidha, Chuo hicho kitajengwa na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China.
Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo ameishukuru Serikali ya Watu wa Jamhuri ya China kwa msaada wa Ujenzi wa Chuo hicho na kuahidi kuendeleza ushirikiano ulioanzishwa na waasisi wa nchi hizo mbili ambao ni Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mao Tse-tung wa Jamhuri ya Watu wa China.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.