Mkuu wa Utumishi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli amefunga rasmi mafunzo ya JKT kundi maalum la kwa mujibu wa sheria kwa waheshimiwa Wabunge na watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Operesheni Jenerali Mabeyo.
Meja Jenerali Simuli amewasihi waheshimiwa Wabunge na watumishi wa Bunge waliohitimu mafunzo hayo kukiishi kiapo chao ili kulijenga taifa la Tanzania.
Amesisitiza umuhimu wa uzalendo pindi wawapo maofisini mwao pamoja na kumuunga mkono Mhe. Rais na Amir Jeshi Mkuu katika kuijenga nchi.
Mafunzo hayo yalijumuisha masomo ya ujanja wa porini, silaha, mbinu za kivita, utimamu wa mwili, uzalendo, historia ya JKT na JWTZ pamoja na ukakamavu.
Mafunzo hayo ya majuma manne yalifunguliwa rasmi tarehe 05 Julai 2022, katika Kambi ya JKT Makutupora Dodoma yakiwa na Wabunge 21 na watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 18.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.