 
         
         Posted On: Friday, 4th August 2023
            Posted On: Friday, 4th August 2023 
        Wahariri wa Habari hapa nchini wametakiwa kuimarisha usalama na umoja wa kitaifa kwa kutokuandika habari zenye uchochezi na uvunjifu wa amani wa Taifa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Fatma Rajab kwa niaba ya Mhe. Tabia Maulid Mwita Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar alipokuwa akifunga kozi fupi ya 15 /2023 ya wahariri wa habari Tanzania iliyoendeshwa na Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi kilichoko Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa mafunzo waliyoyapata yawasaidie kufanya tathmini ya kina kila wanapohariri na kuchambua habari zenye tija na maslahi mapana ya Tanzania.
"Muende mkaoneshe tofauti kati yenu na wanahabari ambao hawana kozi hii ili kuifanya nchi ya Tanzania kustawi zaidi" alisisitiza Waziri Mwita.
Kozi hiyo iliongozwa na kauli mbiu isemayo Nafasi ya Vyombo Vya Habari katika Kuimarisha Usalama na Kukuza Umoja wa Kitaifa imewajumuisha wahariri 59 kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya serikali ,taasisi na binafsi.
 
                         
                         
                         
                        Tanzania People's Defence Forces,
 
P.O.Box 194  Dodoma,
            
Street : Miyuji, Msalato
            
 Fax : +255 26 2962123
            
 Tel : +255 737 962 064
            
E-mail :  ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.