Mkutano wa Wakuu wa Usalama na Utambuzi wa Afrika na Marekani umefunguliwa rasmi tarehe 01 May 24 jijini Dar es Salaam, kujadili mambo mbalimbali likiwemo suala la ugaidi Afrika na Duniani kwa ujumla.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Dkt. Mbaraka Naziadi Mkeremy amesema kuwa dhumuni la mkutano huo ni kujadili kwa pamoja namna nzuri ya kukabiliana na tatizo la ugaidi, mabadiliko ya tabia ya nchi, wahamiaji haramu na mengineyo ili kuifanya Afrika kuwa sehemu salama kwa ajili shughuli mbalimbali.
Nae mwakilishi kutoka Jeshi la Marekani Brigedia Jenerali Rose Keravuori amesema kuwa nchi yake ipo tayari kushirikiana na Majeshi ya Afrika katika kukabiliana na masuala hayo kuanzia ngazi ya awali kabisa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.