Aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania, Balozi Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed leo tarehe 23 Agosti, 2021 amemkabidhi ofisi Mnadhimu Mkuu anayechukua nafasi yake, Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule.
Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato jijini Dodoma.
Makabidhiano hayo yamefanyika kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua na kumuapisha Balozi Luteni Jenerali Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania nchini Uturuki na nafasi yake kuchukuliwa na Luteni Jenerali Mathew Mkingule.
Mapema leo kabla ya makabidhiano kufanyika, Mnadhimu Mkuu mpya Luteni Jenerali Mathew Mkingule alikagua gwaride maalum la mapokezi ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kwa cheo na madaraka aliyonayo kwa sasa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.