Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman ameanza kazi rasmi tarehe 04 Julai 2022 baada ya kufanyika makabidhiano na aliyekuwa mtangulizi wake Balozi Mteule Luteni Jenerali Methew Edward Mkingule.
Makabidhiano hayo rasmi yamefanyika ofisini kwa Mnadhimu Mkuu Makao Makuu ya Jeshi (MMJ) Msalato Jijini Dodoma. Luteni Jenerali Othman ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 29 Juni 2022 na kuapishwa tarehe 30 Juni 2022.
Luteni Jenerali Othman kabla ya uteuzi huo alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.