Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax leo February 23, 2022 amekabidhi Leseni za Urubani kwa Maafisa 20 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliomaliza mafunzo yao nchini Afrika Kusini Novemba 2021.
Aidha, Dkt. Stergonena Tax amesema Marubani hao ni hazina kwa JWTZ, Wizara ya Ulinzi na JKT na Taifa kwa ujumla ambao wataliletea heshima Jeshi na Taifa la Tanzania. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, pamoja na Maafisa na Askari. Akizungumza katika hafla hiyo, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ amewataka marubani hao kuzingatia mafunzo waliyopata na kutumia ujuzi huo katika utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi na weledi ili kuleta tija kwa Jeshi na Taifa kwa ujumla.
Vilevike, Luteni Jenerali Mkingule alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simba, Bi. Erika Rubin na ujumbe wake kutoka Afrika Kusini kwa kuratibu na kuendesha Mafunzo hayo nchini humo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.