Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Innocent Lugha Bashungwa Leo tarehe 17 Juni 2023 ametunuku Shahada ya Uzamili na Shtashahada ya Mafunzo ya Ulinzi na Usalama kwa Maafisa jumla 65 waliokuwa wakisoma kwenye Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo Duluti Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Awali Wanahitimu wote walitunukiwa Beji ya Ukamanda na Unadhimu na Mkuu wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Sylvester Ghuliku.
Waziri wa Ulinzi
Mhe.Bashungwa amewataka wahitimu hao kwenda kuitumia elimu walioipata kutatua changamoto mbalimbali za kiusalama na kulinda uhuru na maslahi mapana ya nchi zao.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Faraja Mnyepe, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Othman ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa vyuo vya Ukamanda na Unadhimu wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na Waambata Jeshi.
Kundi la 37 la kozi hiyo lilijumuisha Maafisa toka Afrika kusini, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Eswatini, Kenya Malawi, Misri, Msimbiji, Nigeria, Rwanda Tanzania na Uganda.Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.