Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMh. Kassimu Majaliwatarehe 13 Agosti, 2018 alifungua rasmi kozi fupi ya tano ya uongozi katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
Jumla ya washiriki 23 kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, NIDA, DIT na Vyombo vya Habari wanahudhulia kozi hiyo.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi hiyo aliwataka washiriki kuzingatia mafunzo yatakayotolewa wakati wote wa kozi ili yaweze kuleta tija kwa Taifa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 9203 Dar es Salaam,
Street :Magore, Upanga
Fax : +255 22 2153432
Tel : +255 22 2150592- 4
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.