Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Kanali Ramadhani Dogoli amezungumzia ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP) utakaofanyika kesho tarehe 8 Mei, 2018 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliofika Makao Makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar es Salaam, Kanali Dogoli amesema mashindano hayo yapo katika mzunguko waTano (5) na yatafanyikampaka Mei 18, 2018 katika Uwanja wa Uhuru na viwanjavilivyopo katika Kambi ya Jenerali Abdalah Twalipo, Mgulani.
Kanali Dogoli amesema kuwa michezo itakayoshindaniwa ni Mpira wa Miguu kwa Wanaume, Mpira wa Pete kwa Wanawake, Mpira wa Kikapu kwa Wanaume na Wanawake, Mpira wa Wavu kwa Wanaume na Wanawake, Mpira wa Mikono kwaWanaume na Wanawake, Ngumi za Ridhaa kwa Wanaume, Riadha kwa Wanaume na Wanawake na Ulengaji Shabaha kwa Wanaume na Wanawake.
Washiriki wa Mashindano hayo ni Wanajeshi kutoka KamandizaJWTZ ambazo ni Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi (NGOME), Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu(Nyika), Kamandi ya Jeshi la Anga (AFC), Kamandi ya Jeshila Wanamaji (NC) na Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Mgeni rasmi siku ya ufunguzi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. HarissonGeorge Mwakyembe (MB).
Hakutakuwa na Kiingilio, Wananchi Wote mnakaribishwa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.