Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Innocent Lugha Bashungwa ametembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi inayojengwa Msalato Jijini Dodoma.
Mhe. Waziri Bashungwa akiwa ameongozana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman amejionea maendeleo ya ujenzi na kusema kuwa, ujenzi umefikia hatua nzuri na ameridhika na hatua hiyo.
Aidha, Mhe. Waziri amepongeza jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha Jeshi kuwa na Hospitali kubwa ambayo itasaidia kuwahudumia Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma na wananchi.
Pia, amewapongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman kwa kufanikisha mradi wa Hospitali hiyo.
Ujenzi wa Hospitali hiyo unafadhiliwa na Jeshi la Ujerumani chini ya Shirika la GAFTAG kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.