Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Elias Kwandikwa ameipongeza Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kusaidia wanawake wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshirikiulinzi wa amani.
Waziri Kwandikwa amesema hayo leo katika kituo cha ulinzi wa amani (PTC) jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa vifaa hivyo na Balozi wa UAE Mh. KhalifaAbdulrahman
Amesema Wizara itaendelea kuwashirikisha wanawake katika mambo mbalimbali kama ilivyo katika sekta nyingine hivyo aliwataka wazazi kuendelea kuwaunga mkono watoto wao wa kike ili kulitumikia taifa.
Kwa upande wake Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Mh. Abdulrahman alisema msaada huu ni kutambua mchango wa wanawake katika ulinzi wa amani.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed alisema msaada huu utasaidia kuongeza nguvu katika mahitaji ya wanawake hao walinda amani ambayo wamekuwa wakipatiwa.
Kwa upande wake mwakilishi wa walinda amani wanawake Meja Justina Gessine alisema wanawake walinda amani hukabiliwa na changamoto za kimazingira kutokana na hali zao lakini anashukuru Jeshi na wadau wengine kusaidia kuziondoa na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.
Sherehe za kukabidhi msaada huo zilihudhuriwa na Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Alfred Kapinga, Mwakilishi mkazi wa Umoja wa MataifaZlatan Milisic, Mkurugenzi wa Jenda kutoka wizara afya mboni mgaza na macocha tembele kutoka wizara mambo ya nje.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.