Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax amefanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Tanzania yaliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam tarehe 12 Octoba 21.
Mheshimiwa Waziri ametembelea Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake anazozifanya za kutembelea Kamandi za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Brigedi, Vikosi, vyuo pamoja na shule kwa lengo la kujitambulisha, kujionea utayari kiutendaji, pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo kiutendaji katika kulinda mipaka ya nchi yetu.
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mheshimiwa Waziri ameipongeza Kamandi kwa kufanya kazi kwa weledi na uhodari mkubwa.
Naye Mkuu wa Kamandi ya Wanamaji Rear Admiral Michael Mumanga amemshukuru Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa kuitembelea Kamandi ya Wanamaji na kujionea utendaji kazi wa Kamandi.
Katika ziara hiyo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aliambatana na Kamishna wa Utafiti na Maendeleo ya Jeshi Meja Jenerali Salum Othman.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.