Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. John Elias Kwandikwa (Mb) amefanya ziara na kukagua ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa yaliyopo Kikombo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 05 Machi 2021.
Mhe. Waziri alipongeza jitihada zinazofanywa na JWTZ chini ya kikosi kazi cha ujenzi kinachojumuisha Maafisa, Askari na Vijana wa JKT kwa kutanguliza uzalendo kutekeleza majukumu ya kitaifa..
Naye Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yacoub Mohamed alitoa shukrani zake kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi kwa Mhe. Waziri kwa kufanya ziara eneo la Kikombo mahali ambapo Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa yanajengwa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.