Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Hussein Mwinyi leo Julai 28, 2018 amewatunuku nembo ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania na vyeti kwa ngazi ya Stashahada na Shahada ya Uzamili ya Usalama na Stratejia jumla ya wahitimu thelathini na moja kwenye mahafali ya sita yaliyofanyika chuoni hapo Kunduchi, Jijini Dar es Salaam.
Aidha Waziri Mwinyi amesema ana uhakika wahitimu wamejifunza maadili na uongozi na pia masuala ya usalama na stratejia hivyo amewataka wakawe mabalozi wazuri katika nchi zao ili kuendeleza sifa nzuri ya chuo.
Mahafali ya sita ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, JWTZ, Mabalozi na Waambata Jeshi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.