Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT ) Dkt Hussein Mwinyi (MB) leo amewasili rasmi Mkoani Mtwara katika moja ya ziara yake kuona maendeleo ya Operesheni Korosho ambayo inasimamiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Aidha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Yakubu Mohamed, akiambatana na Msimamizi Mkuu wa Operesheni hiyo, Meja Jenerali George Msongole pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Manda walimkaribisha Waziri Dkt Hussein Mwinyi katika kiwanja cha ndege cha Mtwara na kuanza ziara ya kutembelea maeneo ambayo Operesheni Korosho inaendelea katika maeneo tajwa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Opereshen Korosho Kanali Benjamin Kisinda alisema kuwa zoezi la ubebaji korosho limeshaanza kwa kuhamisha korosho hizo kutoka katika Maghala yaliyokwisha jaa na kuzipeleka katika maghala elekezi ili kupisha upokeaji wa korosho kutoka katika vyama vya wakulima.
Pia Kanali Kisinda alisema kuwa usafirishaji huo umezingatia zaidi maeneo ambayo maghala yamekwisha jaa na barabara zake sio kiwango cha lami zikiwemo Wilaya za Tandahimba, Newala, Masasi, Nachingwea na Liwale.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.