Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mh. Dkt. Hussein Mwinyi akabidhiwa ukuta wenye urefu wa kilomita 14.4, unaozunguka uwanja wa ndegevita ulioko Ngerengere Mkoani Morogoro leo tarehe 20 Agosti, 2018.
Sherehe za makabidhiano hayo zilifanyika katika kikosi cha Ndegevita kilichopo Ngerengere. Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Mwinyi ametaka ukuta huo kutunzwa kwani utawasaidia makamanda kulinda miundombinu kambini pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa usalama.
Baada ya kuupokea ukuta huo, Dkt. Hussein Mwinyi aliukabidhi rasmi kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ). Kamandi ya Anga.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.