Waziri wa Ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Lieberman amewasili nchini kwa ziara ya kikazi Machi 20, 2018 ambapo leo Machi 21, 2018 amefanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi ofisini kwake.
Katika hatua nyingine Waziri Lieberman ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo ofisini kwake Upanga jijini Dar es salaam.
Ziara ya Waziri huyo imelenga kudumisha Uhusiano baina ya Tanzania na Israel hasa katika nyanja ya Ulinzi na Usalama.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.