Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.John Pombe Magufuli amefunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' lililofanyika siku ya Ijumaa tarehe 30 Septemba katika Kijiji cha Baatini Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani
Zoezi hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha kamandi zote tano za JWTZ ambazo ni Ardhini, Majini, Anga, Kamandi ya Makao Makuu na Jeshi la Kujenga Taifa limefanyika katika ufukwe wa bahari ya Hindi na limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita kwa kukomboa eneo fukwe lililotekwa.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ walioshiriki katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini, uhakika na weledi wa hali ya juu.
''Kwa kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo yote, hii mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika'' amesema Dkt. Magufuli.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.