Mkuu wa Majeshi ya India Admiral Sunil Lanba ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi mapema leo amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo na kukagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vilivyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Akiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mkuu wa Majeshi ya India alipata fursa ya kukutana na Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Hussein Mwinyi (Mb) ofisini kwake, na baadaye kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi nchini ofisini kwake.
Mkuu wa Majeshi anatarajiwa kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mkuu wa Majeshi wa India kufanya ziara hapa nchini na lengo la ziara hiyo ni kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.