Mwenyekiti wa Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, amefanya ziara katika mpaka wa Kusini mwa Tanzania. Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, Mkurungezi Mkuu wa Usalama wa Taifa CP Diwani Athmani, Kamishnawa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala walifanya ziara ya kutembelea mpaka wa kusini katika vituo vya Mnazi Bay, Kilambo, Kitaya na Mtambaswala kuanzia tarehe 16 Octoba hadi 17 Octoba 2019.
Akizungumza na wanakijiji wa vijiji vyaKitaya na Mtambaswala, Jenerali Mabeyo aliwakumbusha wanakijiji hao kuwa jukumu la ulinzi wa taifa linaanzia kwa wananchi wenyewe hivyo ni vema wananchi wakatoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama pale wanapoona kuna watu wanao watilia mashaka katika maeneo yao ili hatua stahiki zichukuliwe kwa ajili ya kuzuia uhalifu usitokee.
Aidha Jenerali Mabeyo wakati wa ziara hiyo alinzidua majengo ya Ofisi na madarasa ya Shule ya Msingi iliyopewa jina la Jenerali Venance Mabeyo iliyopo Michiga katika kijiji Pacheni wilayani Namtumbo mkoani Mtwara.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.