Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Meja Jenerali Shabani Balaghash Mani amefungua rasmi zoezi la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania lijulikanalo kama Dragon Fly katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Meja Jenerali Mani amesema zoezi hilo linalenga kuimarisha ulinzi wa anga ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema hivi sasa Tanzania inaboresha miundombinu yake hivyo haina budi kuilinda kwa gharama yoyote ile.
Zoezi hilo limehusisha zana vita ambazo ni ndege vita, helkopta, makombora ya masafa ya kati, makombora ya masafa mafupi, mizinga ya kutungulia ndege pamoja na zana za uchunguzi ikiwa ni pamoja na rada.
Zoezi hilo ni muendelezo wa mazoezi mbalimbali ya kivita yanayofanyika hapa nchi lengo likiwa ni kuwaimarisha wanajeshi zaidi ili kutimiza majukumu yao ya kiutendaji kwa ueledi zaidi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.