Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda amefunga rasmi zoezi la kivita KAA TAYARI lililokuwa linafanyika katika misitu ya Nyahua Wilayani Sikonge Mkoani Tabora.
Jenerali Mkunda wakati wa kufunga zoezi hilo lililoshirikisha Majeshi ya nchi kavu, Angani, Majini, JKT na Jeshi la Akiba (Mgambo) amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa kudhamilia kuliboresha Jeshi kwa kulipatia zana za kisasa.
Jenerali Mkunda amevisisitiza Vikosi vyote kufanya mafunzo na mazoezi kwa nguvu zote ili kujiweka tayari katika kutekeleza majukumu ndani na nje ya nchi wakati wote wa Amani na Vita.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.