Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (Mbunge) amefungua rasmi zoezi la Medani la Majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lijulikanalo “Ushirikiano Imara 2018” leo Mlingano, jijini Tanga.
Zoezi Ushirikiano Imara 2018 limeshirikisha Majeshi ya Ulinzi, Polisi na Taasisi za Kiraia kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika upangaji na ufanyaji wa pamoja operesheni muhimu katika kutatua changamoto za kisiasa na kijamii.
Akizungumza mbele ya hadhara Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amesisitiza kudumisha mahusiano yaliyo mema na ufanisi katika majukumu ya ulinzi.
Maudhui ya zoezi hilo ni kupambana na ugaidi, kupambana na uharamia, operesheni za ulinzi wa amani na kukabiliana na majanga.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.