Utulivu Afrika ni zoezi la kituo cha Uamrishaji wa utendaji kivita lililoandaliwa na nchi wanachama kutoka katika Jumuiya ya nchi za Afrika (AU) waliojitolea kwa lengo la kuwa na chombo cha pamoja kitakachoweza kutatua matatizo mbalimbali ikiwemo masuala ya ulinzi na usalama kwa nchi wanachama.
Aidha zoezi hilo lililoandaliwa na nchi zisizopungua kumi na tatu kutoka Afrika ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo ikiwakilishwa na maafisa chini ya uongozi wa Brigedia Jenerali Athanasi Mbonye ambaye alikuwa msaidizi wa msimamizi mkuu wa zoezi Meja Jenerali Nakibus Lakara kutoka Jeshi la Wananchi wa Uganda (UPDF).
Zoezi la Utulivu Africa IV CPX 2018 ambalo lilifanyika kwa muda usiopungua siku kumi tangu kuanza kwake leo tarehe 03 Septemba 18 limefungwa rasmi na Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Uganda Mh. Lt col (rtd) Charles Engola katika viwanja vya Gadafi Jinja nchini Uganda
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 9203 Dar es Salaam,
Street :Magore, Upanga
Fax : +255 22 2153432
Tel : +255 22 2150592- 4
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.